Breaking

Friday 25 November 2022

CHANGAMOTO MALEZI YA KAMBO, KUASILI ZATAFTIWA SULUHU

Na WMJJWM Dodoma

Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum imesema ipo katika mchakato wa kupitia upya Sera na taratibu zilizipo kwasasa ili kuweka utaratibu mzuri utaowezesha kupunguza changamoto katika zoezi la Kuasili na Malezi ya Kambo kwa watoto nchini.

Akizungumza katika Kikao kazi cha wadau kutoka Wizara za kisekta na Taasisi za Serikali kilichofanyika Novemba 25, 2022, jijini Dodoma Kamishna wa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt Nandera Mhando amewataka wadau hao kuja mapendekezo ya namna bora za kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika mchakato wa Kuasili na Malezi ya Kambo kwa watoto nchini.

Aidha Dkt. Nandera amesema kuna umuhimu wa kupitiwa na kuangaliwa upya kwa sera na taratibu za kuasili watoto kurahishwa zoezi hilo kutokuwa na changamoto nyingi zitakazosababisha kuchukua muda mwingi kwa Watoto wenye huhitaji wa Malezi ta Familia kuungana na familia hizo.

“Watoto wapo wengi wenye  uhitaji wa kusaidiwa katika Jamii zetu hivo inabidi changamoto  zinazokwamisha  mchakato wa watoto hao kuasiliwa zitatuliwe ili kurahisha huduma ya Malezi ya Kambo na kuasiliwa” alisema Dkt. Nandera.

Kwa upande wake Kamishna wa Ustawi wa Jamii Msaidizi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Baraka Makona          amewataka wadau hao kutoka Wizara  na Taasisi zinazohusika na Huduma ya kuasili pamoja na Malezi ya Kambo nchini kubainisha changamoto zilizopo katika mchakato wa zoezi hilo na kuja na njia ya kuzitatua kwa uharaka zaidi.

“Lengo ni kuwasaidia watoto kupata malezi yanayofaa hivyo pale wanapojitokeza watu wanaotaka kuwasaidia kwa kuwaasili au kwa kuwapatia malezi ya kambo pasiwe na changamoto zinazokwamisha mchakato huo” alisema Kamishna Msaidizi Baraka


Aidha Afisa Ustawi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Zaka Olais  amesema changamoto zinazokwamisha suala zima la kuasili au malezi ya kambo kwa watoto ni pamoja na kucheleweshwa kwa uchunguzi kutoka Idara ya uhamiaji kwa Raia wa nje wanaotaka kuasili watoto pamoja na kukosekana kwa vigezo maalum  vya kuasili watoto wanoishi katika Makao ya kulelea watoto.

MWISHO.


 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages