Breaking

Saturday 5 November 2022

WATUMISHI WALIOONESHA UDHAIFU USIMAMIZI WA MANUNUZI, MIKATABA KWENYE HALMASHAURI KUCHUKULIWA HATUA




OR TAMISEMI

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Angellah Kairuki amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kuwachukulia hatua watumishi walioonesha udhaifu katika usimamizi wa manunuzi pamoja na mikataba katika Halmashauri.

Amesema hayo Leo tarehe 05 Novemba 2022 Bungeni Dodoma Wakati akijibu hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye taarifa za Kamati za kudumu za Bunge za PIC na LAAC na kueleza kuwa kufikia mwezi Agosti mwaka huu Watumishi 116 wameshachukuliwa hatua.

Waziri Kairuki amesema tayari wamewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakikisha ifikapo tarehe 15 Novemba wanaleta taarifa za hatua zilizochukuliwa kwa watumishi wote walioonesha udhaifu katika usimamizi wa manunuzi na mikataba.

Amesema kuna baadhi ya Watumishi walikuwa wameshahamishwa katika vituo vyao baada ya kubainishwa wamerudishwa katika Halmashauri hizo kwa ajili ya kujibu tuhuma kama ilivyofanyika katika Manispaa ya Ubungo, Rorya na Mwanza.

Aidha, Waziri Kairuki amesema baadhi ya halmashauri zimekuwa zikiiga aina ya miradi kama stendi na masoko bila kufanya upembuzi yakinifu na kuwaitiani na maadiko ya miradi ambapo sasa TAMISEMI imeandaa Mwongozo wa namna ya uandishi wa miradi ya uwekezaji katika Halmashauri.

Katika hoja ya usimamizi wa Mikopo ya Halmashauri, Waziri Kairuki amesema katika mwaka wa fedha 2021/22 tayari zimeazishwa akaunti maalum kwa ajili ya fedha zitakazotolewa na kurejeshwa ziwekwe katika kumbukumbu za Vikundi vinavyokopa mikopo ya makundi maalum ya Wanawake, Vijana na watu Kwenye Ulemavu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages