Breaking

Friday 11 November 2022

MAJAMBAZI WAVAMIA NA KUAMURU KUPIKIWA KUKU KABLA YA KUIBA




Wenyeji wa Kitengela wamelilia asasi za usalama kuwanusuru kutokana na utovu wa usalama unaoendelea kuwakosesha usingizi kila kukicha.

Wenyeji hao wameripoti kuwa majambazi wanaowavamia wana tabia za kiajabu, kwani huwalazimisha kuwapikia mlo kabla ya kuwaibia majumbani mwao.

Mkaaji wa kijiji cha Noonkopir Nchini Kenya alisimulia jinsi simu yake ilivyotwaliwa na kuamrishwa kupika sima na kitoweo cha kuku na majambazi waliomvamia.

Agatha Njogu aliiambia jarida la Nation.africa kuwa alipoendelea kuwapikia wavamizi hao, mmoja wao alikuwa akiwafuatilia yeye na wanao huku wengine wakizidi kuchokora nyumba na kuiba.

"Hawakuwa na haraka. Ni uvamizi uliopangwa kwa makini,” Njogu aliiambia the Nation. Wenyeji wamelaumu ongezeko la visa vya ujambazi, kwa utepetevu wa maafisa wa usalama eneo hilo.

Wanadai kwamba maafisa wa kituo kidogo cha polisi cha Noonkopir, hujitokeza kwa saa chache hata ingawa wanahitajika kwa dharura.

"Tuliamua kuweka kituo kidogo cha polis kwa sababu ya visa vya uhalifu kwenye mtaa wetu. Ila maafisa kwenye kituo hicho huwekwa kwa saa chache kisha huondoka," mzee wa kijiji cha Noonkopir village Clement Njung'e alinukuliwa akisema.




Via: Tuko
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages