Breaking

Saturday 26 November 2022

SEKTA YA GESI MTWARA TPDC KUSHIRIKIANA NA ARA, KUTOA AJIRA ELFU 10 KWA WATANZANIA



Na Richard Mrusha

Waziri wa Nishati,January Makamba, ameliasa Shirika la Maendeleo la Petroli nchini(TPDC) na kampuni ya petroli ya ARA, kuhakikisha mradi wa uchimbaji wa gesi kitalu cha Ruvuma kilichopo mkoani Mtwara unamalizika kwa wakati.

Makamba ameyasema hayo Novemba 25, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa halfa ya uwekaji saini mkataba wa yongeza wa uzalishaji na Ugawanaji Mapato(PSA) kitalu cha Ruvuma-Mtwara.

amesema dhamira ya serikali ni kuona mradi huo unakuwa na tija kwa wananchi wanaozunguka eneo la mradi na kupata fursa ya ajira ambayo italeta chachu ya maendeleo katika eneo hilo na kuweza kutoa ajira 10000 kwa watanzania.

Pia amesema anataka kuona unakamilika ndani ya miezi 12 na hategemei kusikia mradi huo unachelewa kwa kile kinachotajwa kuwa Fedha wakati fedha ya mradi ipo.

Makamba amesema mradi huo ukikamilika utakuwa mradi wa kwanza wa gesi kwa ukanda wa Afrika mashariki ambao utalinufaisha taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo kupata kodi,tozo,Gawio kwa serikali,pamoja na serikali kupata kwenye maligafi.

Aidha,Makamba amesema pia wananchi wa mikoa ya kusini wanatarajia kunufaika wakati wa ujenzi wake ikiwemo kupata ajira wakati ujenzi wa mradi huo,

Na kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa ARA petroleum Erhan Saygi ameishukuru serikali ya tanzania hususa ni viongozi wa serikali za vijiji kwa ushirikiano walioonyesha na kuongeza kuwa kukamilika kwa uwekezaji huo kutachagiza uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali pamoja na kuongeza ajira kwa watanzania hali itakayosaidia kukuza pato la wananchi na taifa kwa ujumla

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa shirika la maendeleo ya petroli Tanzania (TPDC) Dkt. James Mataragio amesema kuwa uwekezaji huo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 500 unatarajiwa kuzalisha takribani futi za ujazo milioni 160 kwa siku huku akiweka wazi kuwa utekelezaji wake utasaidia kuongeza chachu na kushawishi wawekezaji wengi zaidi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages