Breaking

Saturday 19 November 2022

TRAFIKI AMUIBIA MCHINA SHILINGI MILIONI MOJA



Maafisa kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI) wanachunguza kisa ambapo raia mmoja wa Uchina aliripoti kuibiwa shilingi milioni moja na polisi wa trafiki jijini Nairobi.

Raia huyo wa Uchina kwa jina Liz Zhixin anasema kuwa alisimamishwa na maafisa wawili wa polisi wa trafiki katika barabara ya Othaya Alhamisi usiku akitoka Westlands kuelekea Junction Mall.

Kwa mujibu wa Zhixin, aliposimama mmoja wa maafisa hao wa polisi alifungua mlango wa nyuma wa gari lake aina ya Toyota Land Cruiser alikokuwa ameweka pesa hizo.

Afisa huyo kisha alichukua shilingi milioni moja na kuingia katika gari lao aina ya Fielder kabla ya kuondoka mara moja na kuacha nyuma kofia ya mmoja wa maafisa hao wa trafiki.

Zhixin alipiga ripoti katika kituo cha polisi cha Muthangari na kumpokeza wakili wake kofia hiyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages