Breaking

Saturday 12 November 2022

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZA SERENGETI SAFARI MARATHON KUJIKWAMUA KIUCHUMI




Wananchi wanaoishi Kanda ya Ziwa wametakiwa kutumia ipasavyo fursa zinazotokana na mbio za Serengeti Safari Marathon zinazofanyika kila mwaka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujikwamua kiuchumi.

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa kuhitimisha mbio za Serengeti Safari Marathon 2022 katika eneo la Geti Ndabaka Wilaya ya Bunda mkoani Mara.

" Tunataka fursa zisambae ili kila mmoja aone umuhimu wa Hifadhi hii" Mhe. Masanja amesisitiza

Amesema ni vyema kuandaa mazingira mazuri ya kuvutia watalii wanaokuja nchini hasa kutokana na hamasa iliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kupitia Filamu ya The Royal Tour.

"Tunatambua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan amezindua filamu ya Royal Tour lengo ikiwa kuvutia watalii na wawekezaji,hivyo bila ya sisi kuandaa mazingira mazuri hatutaweza kuwapokea vizuri watalii hao" Amesisitiza.

Aidha, ametoa wito kwa Wakuu wa Wilaya wa Mikoa ya Simiyu,Mara,Geita na Mwanza kuzishirikisha jamii katika kufungua fursa zilizopo Kanda ya Ziwa ikiwa ni pamoja na fursa za uvuvi,mazao ya samaki,mazao ya wanyama wa kufuga,kilimo cha mboga mboga na fursa za uwekezaji.

Mhe. Masanja amewaasa waandaaji na washiriki wa mbio hizo kutokata tamaa bali kujenga mshikamano utakaofanikisha ipasavyo mashindano hayo ili kumuunga mkono Mhe.Rais katika kampeni ya Kutangaza Utalii na uwekezaji kupitia Royal Tour.

Naye, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mara,Mhe. Dkt.Halfan Haule ambaye pia ni Mkuu Wilaya ya Musoma amewataka washiriki wa mbio hizo kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ili kujionea vivutio vilivyoko ndani yake

Kwa upande wake Mwakilishi wa Waandaaji wa Mbio za Serengeti Safari Marathon, Timothy Mdinka amesema mwaka huu mbio hizo zimelenga kuitangaza Royal Tour kwa kuiweka slogan hiyo katika jezi na maonesho ya utalii.

"Mbio hizi za Serengeti Safari Marathon ni za Maendeleo na ni tofauti na marathon za aina yoyote Ile kwa sababu mbio hizi zinatoa

fursa ya kukutana wadau wa utalii na kuangalia jinsi gani tutaboresha maisha katika eneo la Serengeti kwa kusimamia msemo wa _Serengeti shall never die_
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages