Breaking

Tuesday, 29 November 2022

WAZIRI MKUU AWATAKA DAWASA KUTAFUTA VYANZO VIPYA VYA MAJI
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuendelea kutafuta vyanzo vipya vya maji na kuviingiza kwenye mfumo.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo Jumanne Novemba 29, 2022 wakati akikagua mradi wa maji Kisarawe mjini na kueleza kuwa kuwa licha ya kuongezeka kwa kiwango cha maji kwenye mfumo wa uzalishaji na usambazaji, wasilale bali waendelee kuwatumia wataalam wa ndani kutafuta maji zaidi.

Amesema kuwa kumekuwa na ongezeko la makazi, viwanda na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji uwepo wa maji ya kutosha.

“Tusilale tuendelee na uzalishaji wa maji, Tunataka huduma hii isambae na iwafikie watu wote”

“Ndugu wafanyakazi wa DAWASA mnapaswa kutambua maji ni huduma nyeti kwenye maisha ya binadamu, kazi yenu inahitaji uaminifu na uadilifu mkubwa, fanyeni kazi hii ya umma, wahudumieni watanzania, tambueni maeneo yenye uhitaji na mpeleke huduma” amesisitiza Waziri Mkuu

Pages