Breaking

Thursday, 1 December 2022

ABIRIA AZUA TAHARUKI AKIJARIBU KUFUNGUA MLANGO WA NDEGE IKIWA ANGANIHofu ilizunguka miongoni mwa abiria waliokuwa wakisafiri kwa ndege moja baada ya mmoja wao kujaribu kufungua mlango wa ndege ikiwa angani.

Abiria huyo wa kike aliinuka na kuanza kuambia wenzake kwamba Yesu alikuwa amezungumza naye na kumtaka kufungua mlango huo mara tu ndege ilipopaa angani.

Ililazimu ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Ohio kutoka Houston kuelekezwa eneo la Arkansas na kutua eneo Little Rock.

Kwa mujibu wa kituo cha ABC News, abiria huyo mwenye umri wa miaka 34 kwa jina Elom Agbeninou alizua kioja huku wahudumu wa ndege wakijaribu kumkabili.

Ilikuwa ni hali ya kisanga na wasiwasi huku Elom akidai kwamba alikuwa na matatizo ya kupata hewa .

Baada ya ndege hiyo kutua katika uwanja wa Little Rock, maafisa walimkamata na kuanza mahojiano kuhusu alichokifanya.

"Alikuwa amesema kwamba alikuwa na matatizo ya kupata hewa akiwa ameketi na ndipo akaamka. Baadaye alisema alikuwa na mshtuko mkubwa na kwa kawaida hangefanya alichokuwa akifanya," alisema abiria mmoaj aliyeshuhudia kisa hicho.

Ndege ilikuwa imepaa fiti 37000 wakati kisa hicho kilikuwa kikifanyika jambo ambalo liliwapa wengi hofu kubwa.

Mmoja wa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo alisema alimskia Olem akisema ni Yeus aliyemwamuru kusafiri mpaka Ohio na akiwa hewani afungue mlango wa ndege.

Makachero baadaye walitambua kuwa abiria huyo alikuwa ametoka nyumbani kuelekea eneo la Maryland ila hata mumewe hakujua alipokuwa akielekea.

"Tutashirikiana na upande wa mashtaka katika afisi ya mwanasheria mkuu wa Marekani ili kuweza kuchunguza kisa hiki kikamilifu na kuona iwapo atashtakiwa," ripoti ya polisi ilisema.

Pages