Breaking

Thursday, 1 December 2022

WATU WATATU WAKAMATWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MHADHIRI SAUTJeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT) Mwanza, Hamida Mussa (64).

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Desemba 1, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa amewataja miongoni mwa waliokamatwa kuwa ni pamoja na Sara Mwendeshasahani (15) aliyekuwa mfanyakazi wa ndani wa marehemu.

Mwili wa mhadhiri huyo ulikutwa Jumanne Novemba 29, 2022 nyumbani kwake Mtaa wa Buzuruga Mashariki wilayani Ilemela mkoani Mwanza ukiwa umelala sakafuni kifudifudi ukiwa na mtandio shingoni huku mfanyakazi wa ndani wa mhadhiri huyo akidaiwa kutokomea kusikojulikana.


Via: Mwanachi 

Pages