Breaking

Thursday, 1 December 2022

SHULE 24 ZAFUNGIWA KWA UDANGANYIFU, WATAHINIWA 2194 WAFUTIWA MATOKEO MTIHANI WA DARASA LA SABABaraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) leo Desemba 1, 2022 limetangaza matokeo ya darasa la saba kwa mwaka 2022 ambapo limetangaza kufuta matokeo yote ya Watahiniwa 2194 sawa na asilimia 0.16 ya Watahiniwa 1,350,881 waliofanya mtihani ambao wamebainika kufanya udanganyifu katika mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi mwaka 2022.

TAZAMA MATOKEO >>HAPA<<

Akitangaza matokeo ya mtihani wa kumaliza darasa la saba mwaka 2022, Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athuman Amasi amesema pia NECTA imezifungia shule 24 kuwa vituo vya mitihani ya Taifa baada ya kuthibitika kupanga kufanya udanganyifu katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi.


Shule hizo ambazo ni sawa na asilimia 0.13 ya vituo vyote vya mitihani nchini, ndani yake zipo shule maarufu ikiwemo ya Musabe ya jijini Mwanza na St Anne Marie ya jijini Dar es Salaam na shule ya Rweikiza ya mkoani Kagera.


Shule hizo ni Kadama shule ya msingi iliyopo Chato- Geita, Rweikiza (Bukoba), Kilimanjaro shule ya msingi (Arusha) Sahare (Tanga), Ukerewe (Mwanza), Peaceland (Mwanza), Karume (Kagera), Al-hikma (Dar es Salaam), Kazoba (Kagera), Mugini (Mwanza), Busara (Mwanza), Jamia (kagera), Winners (Mwanza), Musabe (Mwanza), Elisabene (Songwe), High Challenge (Arusha), Tumaini (Mwanza), Olele (Mwanza), Mustlead (Pwani).


Pia zipo shule za Moregas (Mara), Leaders (Mara), Kivulini (Mwanza) na St Severine (Kagera).

Aidha Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limezuia matokeo ya watahiniwa 540 kutoka vituo sita vya mitihani ndani ya jiji la Dar es Salaam baada ya kugundulika kufanya udanganyifu.

Wanafunzi hao wanatoka katika vituo vya Joylanda, Castle hill, Green Acress, Maktaba, Great Vision na Mtendeni.


Mtihani huo wa kumaliza elimu ya msingi ulihusisha watahiniwa zaidi ya 1.38 milioni nchi nzima
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages