Breaking

Friday 23 December 2022

NAFASI MPYA ZA KAZI WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA



TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizaraya Elimu, Sayansi na Teknolojia anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi ishirini na tano (25) kama ilivyoainishwa katika tangazo hili.


1.0 MWAJIRI: WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


1.1 MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II (UMEME) - NAFASI 15


1.1.1 MAJUKUMU YA KAZI


i. Kufundisha masomo ya fani ya Umeme katika Vyuo;
ii. Kuandaa mitiririko na mpangilio wa masomo;
iii. Kusimamia masomo ya vitendo;
iv. Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani;
v. Kufanya utafiti wa mahitaji ya mafunzo katika Jamii inayozungukachuo;
vi. Kuandaa muhtasari wa masomo;
vii. Kufanya maandalizi ya namna ya kuendesha mafunzo;
viii. Kuandaa vielelezo vya kufundishia;
ix. Kuendesha mafunzo ya nje ya Chuo (Outreach Programs); na
x. Kutunga, Kusimamia na Kusahihisha mitihani.


1.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya umeme

1.1.3 MSHAHARA:

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C


1.2 MKUFUNZI MSAIDIZI MAENDELEO YA JAMII II (MAGARI) - NAFASI 10


1.2.1 MAJUKUMU YA KAZI


i. Kufundisha masomo ya fani ya Magari katika Vyuo;
ii. Kuandaa mitiririko na mpangilio wa masomo;
iii. Kusimamia masomo ya vitendo;
iv. Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi na kwenye mitihani;
v. Kufanya utafiti wa mahitaji ya mafunzo katika Jamii inayozunguka chuo;
vi. Kuandaa muhtasari wa masomo;
vii. Kufanya maandalizi ya namna ya kuendesha mafunzo;
viii. Kuandaa vielelezo vya kufundishia;
ix. Kuendesha mafunzo ya nje ya Chuo (Outreach Programs); na
x. Kutunga, Kusimamia na Kusahihisha mitihani.


1.2.2 SIFA ZA MWOMBAJI


Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita waliofuzu mafunzo ya Stashahada kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya Magari.


1.2.3 MSHAHARA:
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS C


MASHARTI YA JUMLA.


i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa kwa wale tu walioko kazini.
ii. Waombaji wenye ulemavu wanahimizwa kuwasilisha maombi na kuanisha aina ya ulemavu walionao katika mfumo wa kuombea kazi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa hatua stahiki;
iii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iv. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.


- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective
boards)


vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 04 Januari, 2023.


Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja na vyeti vya elimu. anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa;
KATIBU,
OFISI YA RAIS,
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
S.L.P. 2320 DODOMA.


i. Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal)
kupitia anuani ifuatayo; http://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’)
ii. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.


Limetolewa na;
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages