Breaking

Friday 23 December 2022

NG'OMBE 2035, WATU 6 WAKAMATWA HIFADHI YA TAIFA TARANGIRE



Jeshi la Polisi Kupitia kikosi cha kuzuia na kupambana na wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji Nchini kwa kushirikiana na hifadhi ya Taifa Tarangire limefanikiwa kukamata Ng’ombe 2035 walioingia hifadhini kwa ajili ya kulisha mifugo hiyo ambapo ni kinyume na Sheria.

Akitoa taarifa hiyo december 22, 2022 kamanda wa Polisi Kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo nchini kamishina msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA amesema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa sita kwa kosa la kuingiza na kulisha mifugo hiyo ndani ya hifadhi.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Muliyo Lekashu (25),Moringe Mpeleke (30),Sabaya Sumuni (38), Lemburis Roika (45),Terengo Kondeki (70),Saruni Rosio (43) wote ni wakazi wa Emboreti wilaya ya Simanjiro.


Kamanda Pasua amebainisha kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi na mara baada upelelezi kukamilika watuhumiwa watafikishwa katika vyombo vya sheria.

ACP PASUA ametoa wito kwa wafugaji kufuata sheria za matumizi bora ya ardhi vingine amesema kuwa Jeshi la Polisi halito fumbia macho vitendo vya uhalibifu wa rasmali za taifa.

Kwa uoande mhifadhi mwandamizi katika hifadhi ya taifa Tarangire SC WILLIAM MAREGES amesema wao kama wadau wakubwa wauhifadhi hawato sita kuwachukulia hatua wale wote watakao husika na uharibifu wa rasilmali za taifa.

Ameongeza kuwa wataendelea kuzilinda na kuhifadhi rasilmali za taifa kwa masilahi makubwa ya taifa.

Chanzo: Jeshi la Polisi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages