Breaking

Tuesday 20 December 2022

NAIBU WAZIRI MASANJA ATOA USHAURI KWA WAKANDARASI WENYE MISAMAHA YA KODI



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhe. Mary Masanja (Mb) amekishauri kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa kwamba Mkandarasi anapopata msamaha wa kodi ( VAT) ijumuishe na kodi nyingine zilizo chini ya Halmashauri ili kurahisisha utekelezaji wa miradi.

Ameyasema hayo leo katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza leo.

"Ni maamuzi ya busara tukiamua kufanya maazimio ya kuhakikisha tunakamilisha miradi kwa wakati kwa kuweka utaratibu maalum ambao Halmashauri zitapewa taarifa" Mhe. Masanja amefafanua.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri za Jiji la Mwanzana Wakuu wa Taasisi mbalimbali Mkoani Mwanza.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages