Na John Mapepele
Maelfu ya Wananchi kutoka sehemu mbalimbali nchini wamefurika kwenye Tamasha la Bibi Titi Mohamed linaloendelea Usiku huu Ikwiriri-Rufiji.
Burudani kutoka kwa zaidi ya vikundi 30 kutoka Zanzibar na Tanzania Bara vinatumbuiza.
Tamasha hili limeratibiwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge wa Rufiji Mhe Mohamed Mchengerwa,
Mgeni Rasmi wa Tamasha hili, Mhe. Mary Chatanda ameipongeza Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Kwa kuandaa matamasha ya Utamaduni ambayo yanasaidia kurithisha uzalendo kwa vizazi vya sasa.
Aidha, UWT imempongeza Mhe. Mchengerwa kwa kuthamini mchango wa Bibi Titi na kuanzisha Tamasha hili Kwa miaka miwili sasa.
Tamasha hili ni la siku mbili lilianza jana kwa dua maalum ya kumwombea Bibi Titi Mohamed ambapo leo asubuhi limeendelea kwa kongamano maalum.