Breaking

Wednesday 11 January 2023

NDUGU WADAIWA KUMUUA MWENZAO KWA KIPIGO KISA KUMTUKANA MAMA YAKE MZAZI



Mtu mmoja aitwaye Nelson Mollel (33) mkazi wa kata ya Moivo, Wilaya ya Arumeru na Mkoa wa Arusha amefariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa.

Akithibitisha tukio hilo Palisi Mkoa wa Arusha kamishina Msadizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amebainisha kuwa Uchunguzi wa awali wa Jeshi hilo umebaini kuwa mtu huyo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa ni ndugu zake tarehe 03.01.2023 wakimtuhumu kumtukana mama yake mzazi (jina limehifadhiwa) na kumuibia.

Kamanda Masejo aliendelea kufafanua kuwa baada ya kupigwa, ndugu hao waliendelea kukaa na majeruhi bila kumpeleka hospitali hadi ilipofika tarehe 08.01.2023 alifikishwa hospitali akiwa mahututi na kufariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu.

Amesema kuwa Jeshi hilo linaendelea na upelelezi ili kuwakamata watu wote waliohusika katika tukio hilo ambao walikimbia baada ya kuona hali ya marehemu kuwa mbaya.

Mama mzazi wa marehemu Nelson, Janeth Kimario amesema kijana wake alimtukana Matusi ya nguoni Januari 1, 2023.

Amesema baada ya kutukwanwa ndipo alimwambia baba yake mdogo, Abel Mboya (45) ambaye alifanikiwa kumpata Nelson na kumpeleka porini na kuanza kumchapa fimbo akiwa na watu wengine.

“Lakini adhabu ilikuwa kubwa sana na kweli alistaili kuchapwa ila wamezidisha hadi nimempoteza mwanangu," amesema

Dada wa marehemu, Jackline Elias Mollel amesema mdogo wake amepigwa viboko 280 badala ya fimbo 70 vinavyopaswa kwa mujibu wa taratibu zao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages