Breaking

Sunday 15 January 2023

AFARIKI KWA KUNG'ATWA NA MAMBA


Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Modesta Shido (31) mkazi wa Ubaruku Mbarali alikutwa amefariki kwa kung'atwa na Mamba sehemu Za na kiunoni wakati akioga Mtoni katika Mto Wa Mkoji uliopo katika Kijiji cha Lyala Mkoani Mbeya.

Akithibitisha tukio Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Benjamin Kuzaga amesema limetokea Mnamo tarehe 09.01.2023 majira ya saa Tisa Mchana huko katika Kijiji cha lyala Kata ya Luhanga Mbarali ambapo Chanzo cha kifo ni kuoga Mtoni na kupelekea kung na Mamba katika Mto wa Mkoji.


Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa Wananchi kuacha kuwa na tabia ya kuoga mtoni.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages