Breaking

Wednesday 11 January 2023

ASKARI POLISI AKUTWA AMEFARIKI GESTI



Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi

Jesh la Polisi mkoa wa Arusha limesema kuwa tarehe 08 Januari mwaka huu Jeshi hilo lilipokea taarifa ya matukio ya watu wawili kufariki dunia katika maeneo tofauti tofauti katika Mkoa wa Arusha.

Akitoa taarifa hiyo leo Januari 11 kamanda wa Palisi Mkoa wa Arusha kamishina Msadizi wa Polisi ACP JUSTINE MASEJO amesema kuwa Tarehe 08.01.2023 muda wa saa 08:30 usiku Jeshi la Polisi Mkoani hapa lilipokea taarifa ya uwepo wa mtu mmoja ambaye alifariki maeneo ya nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Mrina Shine iliyopo kata ya Levolosi Jijijini Arusha.

Kamanda Masejo amebainisha kuwa mara baada ya kupokea taarifa hiyo, Polisi walifika eneo hilo na kuukuta mwili huo ambao waliutambua kuwa ni Mkaguzi wa Polisi Stewart Kaino (47) Askari Polisi wa wilaya ya Arumeru.

Aidha amesema kuwa jeshi hilo bado linaendelea na uchunguzi wa kina ili kubaini mazingira mazima ya kifo hicho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages