Breaking

Thursday 26 January 2023

DKT. DUGANGE AAGIZA MILANGO YOTE KUONDOLEWA NA KUWEKWA MIPYA KITUO CHA AFYA BAHI



OR TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange(Mb) ameagiza kuondokewa kwa milango yote na fremu zake na kuwekwa milango mingine mipya yenye ubora katika Jengo la Wagonjwa wa nje na Jengo la maabara katika kituo cha afya Babayu wilayani Bahi.

Ametoa maelekezo hayo Jumatano Januari 25, 2023 wakati wa ziara yake wilayani Bahi mkoani Dodoma ya kukagua ujenzi wa miundombinu ya afya ambapo hajaridhishwa na usimamizi wa fedha katika ujenzi kituo cha afya hicho.

Amesema Mkandarasi kwa gharama zake ndani ya siku 14 kwa kushirikiana na Mganga mkuu na Mhandisi ambao wameshindwa kumsimamia wahakikishe inawekwa milango mingine mipya na fremu zake zenye ubora kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa.

Dkt. Dugange amesema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitoa shilingi milioni 500 kujenga kituo cha afya Babayu lakini pesa hizo zimekosa usimamizi madhubuti na kupelekea majengo kutokamilika kwa wakati na kukosa ubora na viwango vinavyotakiwa.

Amesema katika nyakati tofauti Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na Kamati ya Siasa ya wilaya walitembelea ujenzi wa kituo hicho na kuelekeza milango hiyo kurekebishwa lakini mpaka sasa maelekezo hayo hajatekelezwa.

Aidha, Dkt. Dugange amemuagiza Mkurungenzi wa halmashauri kuhakikisha anasimamia ujenzi wa majengo yote yanakamilika ifikapo tarehe 15 Machi 2023 na kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

Dkt. Dugange amesema Serikali haitamfumbia macho mtumishi yeyote anayekwamisha au atakayeshindwa kusimamia kikamilifu fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa katika eneo lake.

Pia, ameitaka Halmashauri ipitie na kujiridhisha na ongeza halisi la gharama za ujenzi wa majengo ya awamu ya pili ndipo halmashauri iweze kutenga fedha za ndani kukamilisna ujenzi wa majengo hayo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages