Breaking

Friday 6 January 2023

IGP WAMBURA AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA MIKOA



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amefanya mabadiliko ya Makamanda wa Polisi wa mikoa katika kuboresha na kuongeza ufanisi wa utendaji kwenye mikoa mitatu.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Ijumaa Januari 06, 2023 na Msemaji wa Jeshi la Polisi David Misime imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo, IGP Wambura amemhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Muslim kwenda Kitengo cha Mipango Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake ikichukuliwa na Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Alex Mukama ambaye alikuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

IGP Wambura amemhamisha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Theopista Mallya kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe.

Aidha amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Shadrack Masija ambaye alikuwa Afisa Mnadhimu Namba Moja Mkoa wa Simiyu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages