Breaking

Friday 13 January 2023

MVULANA WA MIAKA 17 AKAMATWA KWA KUWAPA MIMBA WANAWAKE 10



Jeshi la Polisi la Jimbo la Rivers Nigeria limemkamata mvulana mwenye umri wa miaka 17 aliyetambulika kwa jina la Noble Uzuchi na Chigozie Ogbonna (29) kwa madai ya kuwapa ujauzito wanawake 10 kwa ajili ya biashara haramu ya kuuza watoto.

Waliokamatwa wengine ni washukiwa wawili wa kike, Favour Bright (30) na Peace Alikoi (40) ambao wamedaiwa kuendesha kiwanda cha watoto katika maeneo ya Obio/Akpor na Ikwerre katika jimbo hilo.

Imeeleza kuwa Uzuchi na Ogbonna walikodiwa ili kufanya mapenzi na wasichana hao na kuwapa ujauzito.

Msimamizi wa Polisi, Iringe-Koko amesema kwamba uchunguzi uligundua kuwa mwathirika anapojifungua, mtoto walimhifadhi na kumlipa mama kiasi cha N500,000 [TZS milioni 2.5] na kwamba baadhi ya watoto waliojifungua awali walikuwa wameuzwa tayari.

“Waathiriwa wote walikiri kwamba walishawishiwa kwa uuzaji haramu wa watoto kwa sababu ya hitaji la kukabiliana na changamoto za kifedha,” ameeleza

Aidha, Askari wa Kitengo cha Ujasusi walivamia nyumba mbili, ambapo wahanga wa biashara ya watoto walikuwa wakihifadhiwa na kufanikiwa kuwaokoa wanawake hao.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages