Breaking

Saturday 7 January 2023

RAIS DKT. SAMIA ATEUA GAVANA BOT, KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Bw. Emmanuel Mpawe Tutuba, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Kupitia taarifa iliyotolewa leo Januari 07, 2023 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Bw. Tutuba anachukua nafasi ya Prof. Florens Luoga ambaye amemaliza kipindi chake.

Aidha Rais Dkt. Samia amemteua Dkt. Natu El- Maamry Mwamba kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ambapo Dkt. Mwamba alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kilimanjaro (KADCO).

Dkt. Mwamba anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel M. Tutuba ambaye ameteuliwa kuwa Gavana wa Benki Kuu.

Taarifa imeeleza kuwa Teuzi hizi zinaanza mara moja.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages