Breaking

Friday 17 February 2023

DKT. MOLLEL ATOA WITO WANANCHI KUJITOKEZA KUPIMA MAGONJWA YA MOYO



Na WAF- DSM

NAIBU Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel ametoa wito kwa Watanzania kujitokeza kupima ili kufahamu hali zao za magonjwa ya moyo ili kutambua tatizo mapema na kuweza kulizuia kabla ya madhara makubwa kutokea.

Dkt. Mollel amesema hayo leo Februari 17, 2023 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa Mkutano wa kwanza wa Shambulio la moyo uliohudhuriwa na Madaktari wa magonjwa ya moyo na Wataalamu we wengine wa masuala ya Afya nchini.

"Wito wangu ni kwamba, suala la kupima moyo lisiwe mpaka usikie tatizo, iwe ni wakati wote, ndio maana tunawataka Wataalamu watembee katika vituo mbalimbali ili kuhakikisha wanapima Watanzania wanaofika katika vituo ili wapate kujua hali zao juu ya ugonjwa wa moyo." Amesema

Sambamba na hilo, Dkt. Mollel ametoa rai kwa wananchi kujenga tabia ya kufanya uchunguzi wa magonjwa hususan magonjwa ya moyo mara kwa mara ilikufanya utambuzi wa mapema utaosaidia katika kutibu tatizo hilo.

Aidha, Dkt. Mollel amesema, Rais Samia amehidhinisha fedha nyingi sana katika uwekezaji kwenye Sekta ya afya ili kununua vifaa tiba vya kisasa vinavyosaidia katika ufunguaji wa kifua kwa kiasi kidogo sana na kutibu tatizo la moyo hali iliyosaidia kupunguza muda wa mgonjwa kukaa hospitali kwaajili ya matibabu.

Nae, Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo JKCI Dkt. Peter Kisenge amesema, dhumuni la kikao hicho cha Wataalamu wa masuala ya mayo ni kubadilishana uzoefu ili kujiimarisha katika matibabu ya magonjwa ya moyo nchini.

Amesema, Duniani kwote zaidi ya watu milioni sita Duniani kwote hupata tatizo la mshtuko ghafla wa moyo ambalo linachangia vifo vingi kwa wananchi hivyo kuwataka.

Mbali na hayo, Dkt. Kisenge ametoa wito kwa wananchi kuepuka kula vyakula vinavyoweza kuchangia magonjwa ya mashambulio ya moyo ikiwemo vyakula vya mafuta mengi, na kuepuka uvutaji wa sigara na unywaji pombe kupita kiasi na kufanya mazoezi walau mara tatu kwa week kwa dakika 30.

Mwisho.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages