Breaking

Monday 6 February 2023

AMUUA HOUSE GIRL, AMCHOMA KISU MAMA YAKE, NAYE AUAWA


Watu wawili wameuawa huku mmoja akijeruhiwa kwa kuchomwa na kisu maeneo ya Magomeni Kagera, Mtaa wa Ludewa

Inadaiwa kijana Erick aliyekuwa akiishi nyumbani kwa mzazi wake amemuua dada wa kazi (Anna) baada kukataliwa kimapenzi na baada ya mauaji Erick akautupa mwili chooni; muda mfupi baadaye akamchoma kisu tumboni mama yake mzazi ambaye alihoji alipo dada wa kazi baada ya kukuta damu zimetapakaa kila sehemu.

Kelele za mama mtu kuchomwa kisu ziliwashtua majirani ambao walifika eneo la tukio na kuanza kumshambulia mtuhumiwa hadi kusababisha kifo chake.


Via: Malunde 1 Blog

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages