Breaking

Monday, 20 February 2023

MAMA, WATOTO MAPACHA WAFARIKI WAKIFUA NGUO MTONI


Familia moja katika kijiji cha Mileng'a, eneo la Bondo kaunti ya Siaya inaomboleza kufuatia kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 35, na watoto wake mapacha.

Katika kisa hicho, Eveline Atieno na wanawe mapacha walikufa maji katika Mto Yala, walipokuwa wamekwenda kufua nguo zao.


Akithibitisha kisa hicho, Chifu msaidizi wa Mileng'a Austin Bunde alisema mume wa Atieno alifika nyumbani na kupata watatu hao hawapo.


Alipowaulizia, alifahamishwa kwamba walikuwa wamekwenda kufua nguo mtoni lakini hakuwapata ila nguo walizokuwa wakiziosha.
Baada ya muda, mwanaume huyo na watu wengine jamaa zake ambao tayari walikuwa wamekusanyika kwenye ukingo wa mto huo, walipata habari kwamba mwili wa mmoja wa pacha hao ulipatikana.


Walianzisha msako wa kuwatafuta wawili waliosali kuupata mwili wa Ateno siku moja baadaye.


Kulingana na mila za Dholuo, miili hiyo miwili itasalia kwenye ukingo wa mto huo hadi tatu utakapopatikana.


Chanzo - Tuko News
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages