Breaking

Wednesday 22 March 2023

'HAKUNA MTU ANAYEPASWA KUACHWA NYUMA KWASABABU YA UKOSEFU WA MAJI'


Mkurugenzi Mkaazi Water Aid Tanzania Anna Mzinga

*************************

Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

SHIRIKA la WaterAid Tanzania imeendelea kusisitiza umuhimu wa usimamizi na uendelevu wa rasilimali zetu za thamani za maji na watoa maamuzi kuchukua hatua katika kukabiliana na tatizo la maji duniani.

Kauli hiyo imekuja wakati leo Machi 22, 2023 Dunia ikiadhimisha Siku ya Maji Duniani na kauli mbiu ya mwaka huu inasema "Kuhakikisha Upatikanaji wa Maji katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.

Akizungumzia Siku ya Maji Duniani nchini Tanzania, Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la WaterAid, Anna Mzinga, amesema WaterAid, wataendelea kushirikiana na washirika ili kuunga mkono na kushawishi sera na bajeti na kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa huduma salama, nafuu, zinazozingatia jinsia, jumuishi kijamii na endelevu, huduma za maji taka na usafi kwa kila mtu, kila mahali.

"Tunajua kwamba upatikanaji unaotegemewa wa maji na usafi wa mazingira unaosimamiwa kwa usalama, pamoja na desturi na rasilimali za usafi wa kiafya, huwawezesha watoto, familia na jamii kuwa msingi wa kudumu wa kuboresha afya, uchumi imara na fursa kubwa zaidi" amesema Mzinga.

"Huduma za maji na usafi wa mazingira zinahitaji kuendelezwa kwa kiasi kikubwa ili kufikia maendeleo yanayohitajika sana katika afya na ustawi ambayo yatasaidia nchi kujenga uwezo wa kustahimili siku zijazo na kutimiza uwezo wake.

"Maono ya WAT ni ya nchi kama Tanzania ambapo hakuna mwanamke au msichana anayelazimishwa kutembea na kupanga foleni kwa saa nyingi ili kuchota maji."

Mzinga amesema siku hiyo inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa ambayo inataka kuunga mkono kufikiwa kwa lengo la sita la Maendeleo Endelevu: maji na usafi wa mazingira kwa wote ifikapo mwaka 2030.

Aidha, amesema WaterAid Tanzania inatarajia kuzindua mkakati wake wenye matarajio makubwa zaidi wa miaka mitano (2023-2028) Mei 2023 ambao wanaamini utakuwa karibu na kumaliza tatizo la maji na usafi wa mazingira.

Mzinga amesema kila mtu kila mahali watafikiwa na upatikanaji wa huduma za maji kwa wote, endelevu na salama kwa kuzingatia maeneo ya kijiografia ili kushawishi mabadiliko mapana na kuipa kipaumbele WASH katika sekta ya afya ili kuboresha afya ya umma.

Aidha, wanaendelea kushirikiana na washirika ili kuunga mkono na kushawishi sera na bajeti na kuchangia katika kuboresha upatikanaji wa huduma salama, nafuu, zinazozingatia jinsia, jumuishi kijamii na endelevu, huduma za maji taka na usafi kwa kila mtu, kila mahali.

Amefafanua maoni ya WAT ni ya nchi kama Tanzania ambapo hakuna mwanamke au msichana anayelazimishwa kutembea na kupanga foleni kwa saa nyingi ili kuchota maji.

Aidha amesema wanatamani kuwa mahali ambapo hakuna jamii inayorudishwa nyuma na magonjwa yasiyo kwisha yanaosababishwa na miondombinu mibovu ya maji taka, afya na usafi wa mazingira.

Ametumia nafasi hiyo kueleza WaterAid Tanzania, kila kitu wanachofanya kinalenga kuhakikisha watu walio katika mazingira magumu zaidi kupata maji safi."Tunafanya hivi kwa kusaidia sekta kuondoa baadhi ya changamoto muhimu zinazowakabili ili kufikia malengo ya sasa ya kitaifa ya WASH."
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages