Breaking

Tuesday 14 March 2023

KAMATI YA BUNGE NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUIPATIA GST MASHINE ZA KISASA ZA UTAFITI WA MADINI NCHINI


Na.Samwel Mtuwa - GST 


Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeipongeza Serikali Awamu ya Sita kwa kuipatia Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) vifaa na mashine za kisasa kwa ajili kuongeza wigo wa  utafiti wa madini nchini.


Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 14 Machi 2023 na makamu  mwenyekiti wa Kamati hiyo Judith Kapinga mbunge wa viti maalum wakati akiongea na vyombo vya habari mapema baada ya kukamilisha ziara hiyo.


Ziara hiyo ya kutembelea maabara za GST kwa ajili ya kujionea utekelezaji wa majukumu ya GST , Mhe.  mbunge Judith Kapinga aliipongeza serikali kwa kuwekeza mashine za kisasa katika kufanya uchunguzi, utambuzi na unjenjuaji wa madini mbalimbali.

" kwa kweli niipongeze Serikali ya Awamu ya Sita kwa juhudi inazofanya katika kuiwekeza  taasisi yetu ya GST kwa kuipatia mashine mbalimbali za uchunguzi , utambuzi na uchenjuaji wa madini " alisema kapinga


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Songwe Philipo Mulugo  ambaye pia ni mjumbe wa Kamati hiyo alishauri  kuwa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2023/2024  GST iongezewe nguvu zaidi ya kibajeti ili kuweza kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.


Kabla ya ziara hiyo kuanza, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba aliwakaribisha wajumbe wa Kamati na kuwashukuru kwa mchango wao mkubwa wanaotoa katika kusimamia GST katika kutekeleza majukumu yake. 


"Ninashukuru sana Kamati hii kwa usimamizi wake nzuri ambao umeendelea kuifanya GST kuboreka zaidi katika  utoaji wa huduma zake." Alisema Dkt. Budeba.


Mapema baada ya utambulisho huo Dkt. Budeba alimkaribisha Naibu Waziri wa Madini

Dkt. Steven Kiruswa kwa ajili ya kuanza ziara hiyo ambapo Dkt. Kiruswa aliishukuru Kamati kwa namna mnavyoendelea kuishauri na kuisimamia Wizara ya Madini kwa ufanisi mkubwa. 

"Sisi tunafarijika sana kwa namna mnavyotusimamia Wizara  na Taasisi zake na tunawakaribisha GST muweze kujione mlichokisoma kwenye taarifa zetu". Aliongeza Dkt. Kiruswa


Katika ziara hiyo wajumbe wa Kamati hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali juu ya utekelezaji wa majukumu ya GST hasa juu ya  uchunguzi wa sampuli za madini katika maabara ya GST.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages