Breaking

Monday 22 May 2023

MKENDA KUFUNGUA MAONESHO YA NANE YA TAFITI NA UBUNIFU UDSM

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda anatarajia kufungua maonesho ya nane ya Utafiti na Ubunifu yanayotarajia kuanza Mei 23 - 25, 2023 katika Viwanja vya Maktaba Mpya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


Akizungumza na Wanahabari Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Utafiti, Prof. Lettice Rutashobya amesema maonesho hayo yenye kauli mbiu "Utafiti na Ubunifu kwa Ustawi wa Uchumi - jamii nchini Tanzania"


Prof. Lettice Rutashobyae amesema kuwa maonesho hayo yatataguliwa na ufunguzi ambapo wazungumzaji watakuwa ni Leticia Lutashobya ambaye ni mbobezi katika masuala ya biashara katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Michael Shirima mwenyekiti na Mwanzilishi wa Presicion Air Tanzania.


Amesema kuwa katika maonesho hayo ya nane wanatarajia kuonesha miradi 99 iliyotokana na maonesho yalifanyika katika ngazi ya vitengo ambapo jumla ya miradi 350 na wakachagua hiyo 99.


"Malengo ya Tafiti hizi ni kuwavutia wanataaluma kutoka chuo chetu na taasisi nyingine zinazohusiana na Taaluma Pamoja na utafiti na watu wote wa serikalini ikijumlisha wenye viwanda kuja kushuhudia tafiti na bunifu zao wanazofanya katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam," amesema Prof. Rutashobya


Ameongeza kuwa tafiti zote zinazofanywa katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam zinalengo la kuboresha maisha ya Watanzania hivyo ni vyema watu wakajitokeza kwa wingi kuhudhuria maonesho hayo ili waweze kujifunza mambo mbali mbali.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages