Breaking

Saturday 17 June 2023

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO JUNI 19


Na Lango la Habari

Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya Jumatatu Juni 19, 2023 kwenda Ikulu ya Magogoni, Dar es Salaam.


 Kupitia taarifa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam SACP Muliro J. Muliro imeeleza kuwa Taarifa hiyo ya mtu mmoja anayodai kuwa aliifikisha Polisi, tayari amejibiwa kwa kuyapiga marufuku maandamano aliyokuwa akitaka kuyaratibu. 


Kamanda Muliro Amesema mtu huyo ameshauri kuwa kama ana jambo la msingi atumie vyombo mbalimbali vya kisheria anavyoweza kufika na kuwasilisha hoja zake bila maandamano ili haki zingine za wananchi kufanya kazi wakiwa huru zisiingiliwe. 


"Jeshi la Polisi linawatahadharisha watu kutoshiriki hicho kinachodaiwa maandamano na badala yake mnahimizwa kuendelea na shughuli zenu za kijamii bila hofu" Amesema SACP Muliro 


Aidha ameongeza kuwa Jeshi La Polisi halitasita kuchukua hatua kwa mtu au kundi la watu kutaka kuzua taharuki kwa kuzuia watu. kufanya kazi zao wengine.


Maandamano hayo ya amani yameitishwa na Kijana Mwanaharakati wa Haki za Binadamu Deusdedith Soka ambapo amenukuliwa akisema lengo la maandamano hayo ni kupinga mkataba wa Bandari kati ya Serikali ya Tanzania na DP World.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages