Breaking

Thursday 1 June 2023

NDEGE YA MIZIGO BOEING 767-300 KUWASILI NCHINI JUNI 3,2023

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI inatarajia kupokea ndege ya kwanza ya kusafirisha mizigo aina ya Boeing 767 -300 mnamo tarehe tatu Juni itakayokwenda kutatua changamoto za usafirishaji wa mizigo kwa wafanyabiashara nchini.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Juni 1,2023 Jijini Dar es Salaam, Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema kukosekana kwa ndege ya mizigo toka nchini kwenda nchi za nje kumechangia ucheleweshwaji wa bidhaa pamoja na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji.

"Zaidi ya Tani elfu 24 za bidhaa ya samaki, mbogamboga na maua toka nchini zimekuwa zikisafirishwa kupitia mashirika mengine hivyo ujio wa ndege hii utatoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kutekeleza majukumu yao kwa urahisi". Amesema Prof.Mbarawa

Aidha amesema tukio hilo la kupokea ndege litafanyika katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi ambaye ataongoza kupokea ndege hiyo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Nae Afisa uhusiano wa Shirika la Ndege Tanzania Bi.Sarah Ruben amewahakikishia wafanyabiashara na wawekezaji nchini kuwa ndege hiyo itakuwa na ratiba maalum itakayotoa fursa kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kuweza kuitumia. Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023

Waziri Wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari leo Juni Jijini Dar es Salaam wakati akitoa taarifa kuhusu ujio wa ndege mpya ya mizigo aina ya Boeing 767 -300 ambayo inatarajiwa kuwasili nchini Juni 3,2023

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages