Breaking

Saturday 3 June 2023

“TGNP” VITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA SULUHISHO LA UKATILI NA CHANZO CHA MAENDELEO



Mkazi wa Kivule Mzee Joseph Gasaya  Mwanachama wa kituo cha Taarifa na Maarifa  akizungumza na baadhi ya Maafisa kutoka Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

*****************

Na Mwandishi Wetu

Wakazi wa kata ya Kivule Jijini Dar es Salaam wameanza kunufaika fursa za na uwepo wa vituo vya taarifa na maarifa  vinavyohusika na kupinga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto vinavyosimamiwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) ambapo  wameanza kukabiliana na  mila na desturi hasi zilizopitwa na wakati kwenye jamii.

Hayo yamebainishwa kwenye kikao cha tathimini ya hali ya utendaji kazi wa kituo cha taarifa na maarifa cha Kata ya Kivule kilichoanzishwa na wakazi hao baada ya kupatiwa elimu na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP)juu ya kukabiliana na vitendo hivyo na namna bora ya kutafuta suluhisho.

Nae Mkazi wa Kivule Joseph Gasaya  mmoja wa wanachama wa kituo hicho alisema kuwa,kituo hicho kimeanza kuleta matokeo chanya kupitia uraghabishaji kwenye jamii umesaidia wananchi kushirikiana na viongozi wa ngazi za mitaa,kata,Jimbo na taifa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

“Tathimini inaonesha wakazi wa Kivule wameelimika kupitia kituo chetu cha taarifa na maarifa na wamekuwa mabalozi wa kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto ambapo kwa sasa vitendo vya ukeketaji vimeaza kupungua ikilinganishwa na hapo awali,tunakemea jamii iondokane na mila hii potofu,”alisema Gasaya.



Awali akichangia hoja katika kikao hicho Husna Membe alisema kuwa TGNP imefanikiwa kuiunganisha jamii kupitia mbinu shirikishi ya  uanzishwaji wa vituo hivi huru  ambavyo kwa sasa vinafanya kazi ipasavyo kwa kushirikiana na viongozi wa  serikali.

“Tukibaini changamoto inayohusiana na ukatili tunashirikiana na wezetu wa serikali  za mitaa na  vyombo vingine  vya kutolea maamuzi kama vile Mabaraza ya usuluhishi ngazi za kata na Mitaa  na ikishindika mashauri hupelekwa kwenye  Mahakama,”alisema Maembe.


Kwa upande wake  mwenyekiti wa Kituo hicho cha Taarifa na Maarifa kata ya Kivule Zahara Mzee amesisitiza kuzingatiwa kwa usawa wa kijinsia katika shughuli za maendele kwenye jamii kwa kutumia mbinu shirikishi ili kuziibua na kuzitatua kero zinazowakabili wananchi ili maendeleo ya eneo hili yaweze kusonga mbele.

 Alisema   Viongozi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa vya kata za  Kivule na Majohe wanashirikiana kwa ukaribu katika Nyanja za maendeleo katika sekta za elimu,afya na miundombinu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kunakuwa na usawa wa kijinsia katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kwenye jamii.

Kwa upande wake Mkazi wa Kivule, Veronica Julius ameyainisha baadhi ya mafanikio wanayojivunia baada ya kuanzishwa kwa kituo hicho mwaka 2022 ambapo waliitisha mkutano ya viongozi wa ngazi ya Kata na Jimbo ambao wamewezesha kutatua kero zao zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

“Tuliomba kuboreshewa huduma za afya katika hospitali ya Kivule  ambayo imepatiwa X-ray Mashine,Ujenzi wa vyoo katika shule za Bombambili na Annex ambavyo ujenzi wake umekamilika,hoja ambazo zimeibuliwa na kituo cha Taarifa na Maarifa kilichojengewa uwezo na TGNP,”alisema  Membe.

Mwisho.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages