Breaking

Wednesday 14 June 2023

WAZIRI MCHENGERWA AFANYA UTEUZI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb) amefanya uteuzi wa Watendaji wawili kushika nafasi mbalimbali kwa mujibu wa Mamlaka aliyopewa kisheria.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Katibu Mkuu wa Maliasili na Utali, Dkt. Hassan Abbasi uteuzi huo unaanza leo Juni 14, 2023.


Kwanza, amemteua Dkt. Florian Geofrey Mtey kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utali - NCT, uteuzi huo ni kwa mujibu wa Amri ya uanzishwaji wa Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) ya mwaka 2003, Kifungu cha 2.2.


Pili, amemteua Kamishna Msaidizi, Salim Athuman Mjema kukaimu nafasi ya Naibu Kamishna wa Huduma za Shirika kwenye Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro NCAA, nafasi iliyoachwa wazi na Needpeace Wambuya aliyehamishwa kituo kingine cha kazi.


Uteuzi huu ni kwa mujibu wa kifungu cha 7 (3) cha Sheria ya Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Sura ya 284 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages