Breaking

Sunday 9 July 2023

WADAU WAKARIBISHWA KUSHIRIKI JUKWA LA KIMATAIFA SEKTA YA MADINI OKTOBA 2023
Wananchi na wadau wanaotembelea maonesho ya Sabasaba wamekaribishwa kupata taarifa kuhusu namna ya kushiriki katika Jukwaa la Kimataifa la Sekta ya Madini kwa kujisajili katika tovuti maalum ya mkutano.

Mratibu wa Jukwaa la Mkutano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Madini Bi. Jacqueline Aloyce amesema kuwa , jukwaa hilo linatarajiwa kuwakutanisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi Oktoba 25 na 26 jijini Dar es salaam.

Amezungumza hayo leo Julai 9, 2023 na kuongeza jukwa hilo litakuwa fursa kwa wenye nia ya kushiriki katika uchumi wa madini, kujifunza, kusikia na kukutana na wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini wanaotembelea banda la Wizara ya Madini katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) Dar es salaam.


Ameongeza kuwa, jukwaa hilo ni fursa kwa wote walio katika mnyororo mzima wa shughul za madini kuanzia wachimbaji wadogo, wa Kati na Wakubwa wa Sekta ya Madini ili kuzungumza kwa pamoja fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta ya Madini.

Ameongeza kuwa, ili kushiriki katika jukwaa hilo muhimu wadau wote wajisajili katika tovuti ya mkutano huo https://www.tanzaniamininginvestmentforum.com

Kwa Mwaka 2023, Jukwaa la Kimataifa Sekta ya Madini inashirikiana na Kampuni ya DMG events na Ocean Business Partners (OBP) katika kuandaa jukwaa la Kimataifa kwenye Sekta ya Madini hapa nchini.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages