Breaking

Thursday 31 August 2023

GST YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA MAONESHO YA MADINI MWANZA



Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) imefanikiwa kuwa Mshindi wa Kwanza na kupata Tuzo katika kipengele cha Taasisi zinazohusiana na Madini.

Tuzo hiyo imetolewa na Chama cha Wafanyabiasha, Viwanda na Kilimo Tanzania (Tanzania Chamber of Commerce, Industry and Agriculture) ambao ndiyo waandaaji wakuu wa Maonesho ya 18 ya Biashara Africa Mashariki yanayoendelea Jijini Mwanza katika Viwanja vya Furahisha.

GST imepata Tuzo hiyo katika maonesho hayo yaliyoanza Agosti 25, 2023 na yanatarajiwa kufikia kilele Septemba 04, 2023 ambayo yanabebwa na Kauli Mbiu isemayo “Mazingira Bora ya Biashara ni kitovu cha kukuza Uwekezaji wa Biashara, Viwanda na kilimo Afrika Mashariki,".

Katika Maonesho hayo, GST imeshiriki kwa kuonesha huduma zitolewazo na taasisi hiyo ikiwemo aina ya miamba ya madini, huduma za maabara, Ramani za maeneo yapatikanayo madini na uchukuaji wa sampuli.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages