Breaking

Thursday 14 September 2023

TIRDO KUENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA MKAA RAFIKI

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania-TIRDO Prof. Mkumbukwa Mtambo ameahidi Shirika lake kuendelea kutoa elimu ya matumizi wa mkaa rafiki katika Mikoa yote ya TANZANIA .
Prof.Mtambo amesema hayo katika hafla ya kufunga mafunzo ya siku tatuna kutoa vyeti kwa wajasiriamali 28 kutoka Mikoa 12 ya Tanzania .

Semina hiyo ililenga kuwajengea uwezo wazalishaji wa mkaa mbadala ili waweze kuongeza uwezo wa uzalishaji wa mkaa Bora.

Semina hiyo imeratibiwa Kati ya TIRDO na REPOA ni muendelezo wa shughuli za TIRDO katika kuendelea kuwaongezea ujezo wajasiriamali katika Sekta mbali mbali za uzalishaji nchini .

Bi Tausi Shabaan Hassan ni mmoja wa washiriki wa semina hiyo ambapo ameahidi kuwa Balozi wa Mkaa Mbadala ili kuendelea kutunza Mazingira.

Mshiriki Mwingine kutoka Mkoa wa Tanga Bw.Abdul-Kheri Kessy ambaye ni mmiliki wa kiwanda cha Aladin Co.Ltd cha Mkoa wa Tanga ametoa wito kwa Serikali kuendelea kuwapa elimu kila mara ili utaalam huu uweze kuwafikia watu wengi.

"Shida kubwa inayotukabili ni utaalam wa kutosha katika uzalishaji wetu ili kufikia masoko ya nje na ndani ya nchi" aliongeza Bw.Kessy.

Bwana Kessy ameongeza kuwa jambo lingine muhimu walilolipata kwenye semina hiyo ni kuongeza wigo kwa mtandao wa uzalisha baada ya kukutana na wadau kutoka mbali mbali na hivyo mbali na ujuzi lakini soko lao pia litapanuka kwa kiasi kikubwa.

Mshiriki Mwingine Bw.Bahati Tweve ameiomba TIRDO kushirikiana na taasisi na Mamlaka zingine kuhakikisha Mashine zinapatikana Kwa urahisi na kwa Bei nafuu.

Mafunzo haya ya kwanza yamehusika Jumla ya washiriki 28 Mikoa 12 ambayo ni Dar es Salaam, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Pwani.

Mikoa Mingine ni Mtwara,Lindi,Tanga,Morogoro,Tabora,Iringa na Mkoa wa Mjini Magharibi Kutoka upande wa Zanzibar .



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages