Breaking

Tuesday 5 March 2024

DAWASA YAPELEKA KICHEKO SALASALA IPTL

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imekamilisha maboresho ya huduma ya Majisafi kwa wakazi takribani 700 katika eneo la Salasala IPTL, katika kata ya Salasala wilaya ya Kinondoni

Maboresho hayo yamelenga kuongeza msukumo wa maji tofauti na ilivyokuwa awali na sasa mradi umekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji kwa uhakika.

Awali katika wananchi katika mitaa ya Amani, Kingdom, Mwarobaini na Transfoma ilikua ikipata maji kwa msukumo mdogo sana, na maeneo mengi kukosa huduma kabisa, lakini kupitia mradi huu changamoto imekamilika kwa kulaza bomba zenye ukubwa wa inchi 2 na 1.5 kwa umbali wa mita 300

Bi. Mwanahawa Hamza mkazi wa mtaa wa Amani ameeleza kuwa adha ya maji waliyoipata awali imetatuliwa na sasa shughuli zao za kila kiuchumi zinakwenda vizuri.

"Hapo awali kabla ya mradi, wakazi wa maeneo haya tulikua hatupati kabisa maji au yakitoka ni kidogo sana, tunashukuru Serikali kupitia DAWASA kwa mradi huu kwani sasa huduma ni nzuri na hudima tunapata wakati wote"ameeleza ndugu Mwanahawa.

Mradi wa uboreshaji huduma ya maji eneo la Salasala IPTL umekamilika kwa asilimia 100 na unanufaisha wakazi wa mitaa ya Amani, Mwarobaini, Transfoma na Kingdom.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages