Breaking

Friday 1 March 2024

MABORESHO MIUNDOMBINU YA MAJI MPIJI MAGOE, KAZI INAENDELEA

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inaendelea na maboresho ya miundombinu ya maji katika eneo la Mpiji Magoe, kata ya Mbweni Wilaya ya Kinondoni.

Kupitia Mkandarasi DB SHAPRIYA & CO LIMITED inatekeleza maboresho hayo yanayohusisha kazi ya kuunga bomba kubwa la kusambaza maji la inchi 54 lililoathiriwa na mvua.

Akizungumzia utekelezaji wa zoezi hilo, Mhandisi Haika Temba amesema kuwa wanafanya kazi ya kutoa bomba la inchi 54 kutoka mtoni na kulichomelea inaendelea eneo la kazi.

"Kazi hii ni endelevu ambapo mpaka sasa kazi ya kuchimba na kutoa maji kwa lengo la kutoa bomba kutoka mtoni inaendelea. Lengo ni kuhakikisha huduma ya maji inaimarika katika maeneo ya Kerege, Mapinga, Mbweni, Tegeta, Bunju Beach, Boko hadi Ununio" amesema.

Mhandisi Haika ameongeza kuwa kazi hiyo inatekelezwa kwa kasi ili kukamilisha haraka matengenezo hayo kabla ya kuanza kwa msimu wa mvua kubwa uliotangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages