Breaking

Wednesday 13 March 2024

WANAGDSS WAJIPANGA KUHAKIKISHA WANAMKOMBOA MWANAMKE KIUCHUMI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WANAWAKE wakiwezeshwa kiuchumi watapata ujasiri wa uthubutu wa kufanya mambo mbalimbali yanayoweza kuchangia maendeleo kwenye jamii inayowazunguka.

Ameyasema hayo leo Machi 13,2024 Afisa wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), idara ya ujenzi wa nguvu za pamoja na harakati, Frola Ndaba wakati wa semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) ambazo hufanyika kila Jumatano katika viwanja vya TGNP Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuna umuhimu mkubwa wa kupashana habari kuhusiana na suala zima la kuzitambua fursa na kujenga ushirika ambao utasaidia kuwainua wanawake ili kuondokana na hali ya utegemezi.

Kwa upande wake, Afisa kutoka Taasisi ya Women and Youth Initiatives, Liberata Kimaro amesema wanawake wanapopata fursa ya kuwezeshwa kiuchumi, jamii hunufaika kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa.

"Mwanamke anapowezeshwa kiuchumi itapelekea kupunguza vitendo vya ukatili hususani kwa watoto na vijana, kutokana na takwimu vitendo vingi vya unyanyasaji vinasababishwa kutokana na kutokuwa na kipato". Amesema 

Naye Mwanaharakati wa Jinsia kutoka Kituo Cha Taarifa na Maarifa kata ya Mabibo, Emmanuel Jigui amesema mwanamke anaathirika kiuchumi kutokana na kupewa majukumu ya kulea familia pamoja na suala la mfumo dume.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages