Breaking

Thursday 6 June 2024

BARRICK YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI 2024 KWA VITENDO

  

Meneja wa Mazingira Mgodi wa Barrick Bulyanhulu (Aliyevaa kofia Nyeupe ) akishiriki zoezi la kupanda miti katika Shule ya Sekondari ya Buyange kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani juzi ambapo wafanyakazi wa Barrick walishiriki zoezi ka kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali.
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhuli wakishiriki zoezi la kupanda miti katika Shule ya Sekondari ya Buyange kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani juzi ambapo wafanyakazi wa Barrick walishiriki zoezi ka kupanda miti na kufanya usafi katika maeneo mbalimbali
Wafanyakazi wa Barrick Bulyanhulu na wanafunzi wa shule ya sekondari Buyange katika picha ya pamoja kabla ya kushiriki zoezi la kupanda miti katika kuadhimisha siku ya Mazingira Duniani.

KAMPUNI ya Barrick nchini kupitia Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu imeshirikiana na jamii inayozunguka mgodi huo kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani mwaka 2024 ambapo wafanyakazi wake wameshiriki kufanya usafi, kukabidhi vifaa vya kufanyia usafi pamoja na kupanda miti.

Katika maadhimisho hayo, mgodi wa Barrick Bulyanhulu umetoa msaada wa vifaa vya kufanyia usafi katika kituo cha Afya Bugarama, miche ya miti ya matunda na kivuli, Mbegu za miche ya miti na kushirikiana na jamii kuipanda katika Shule ya Sekondari ya Buyange kata ya Bugarama Halmashauri ya Msalala.

Akizungumza Baada ya kukabidhi vifaa pamoja na kupanda miti Meneja Mazingira wa mgodi huo, Arespicius Onesmo, amesema wameelekeza shughuli hiyo katika shule hiyo mpya ili kuiboreshea uoto wa asili na mazingira kwa ujumla.“Hii shule ni mpya ina uhitaji ya miti kwa ajili ya kukuza uoto wa asili wa eneo hili,” alisema Ngoloma

“Tumeamua kushirikiana na jamii kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti, na hii inaonesha commitment (uwajibikaji) wa mgodi katika kulinda mazingira.”alisisitiza.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Ambaye ni Afisa Mazingira Halmashauri ya Msalala Humphrey Peter, ameupongeza mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kuthamini maadhimisho hayo na kuona umuhimu wa kushirikiana na jamii kupanda miti ili kulinda mazingira.

“Tunaushukuru mgodi wa Barrick Bulyanhulu kwa kutambua sikukuu za kitaifa na kimataifa. Kati ya taasisi au mashirika yaliyopo katika wilaya yetu ni Barrick Bulyanhulu pekee ndio wanafanya tukio kama hili la siku ya mazingira na wanakuja kusaidiana na jamii kuboresha mazingira,” amesema Humphrey.


Kaulimbiu ya maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani mwaka huu inasema,"urejeshwaji wa Ardhi, ustahimilivu wa hali ya Jangwa na ukame"

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages