Breaking

Saturday 28 September 2024

SARANGA WAPEWA UHAKIKA WA HUDUMA DESEMBA 2024

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Hassan Bomboko amewataka Wananchi wa Mtaa wa Ukombozi katika kata ya Saranga kuwa wavumilivu kwa kipindi kifupi ambayo changamoto ya huduma ya maji na kuahidi ifikapo Desemba 2024 huduma itaimarika kufuatia kukamilika kwa Mradi Mkubwa wa kimkakati wa Bangulo.

Mheshimiwa Bomboko ameyasema hayo katika siku ya tatu ya ziara yake ya mtaa kwa mtaa katika Mitaa na kata za Wilaya ya Ubungo kwa lengo la kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

"Wote ni mashahidi hapa Saranga watu wageuza maisha ya watu mitaji kwa kuwauzia maji na magari kwa bei kubwa sana, Serikali inafahamu changamoto iliyopo lakini zipo juhudi zinafanyika kumaliza changamoto ya hizo ikiwepo utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji Bangulo unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 36.7" ameeleza

Amesema mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 36.7 umefika asilimia zaidi ya 50 ya utekelezaji wake na utakaojibu changamoto nyingi za wakazi wa Saranga, Kinyerezi na maeneo jirani.

Kwa upande wa DAWASA, Mhandisi Zephania Massaga ameeleza kuwa suluhisho la huduma katika ni ukamilishaji wa mradi huo wa kimkakati kwani maeneo mengi yanapata huduma kwa awamu.

"Kwa sasa Mamlaka inaendelea na utekelezaji wa mradi wa maji Bangulo linalohusisha ujenzi wa tenki kubwa la Lita milioni 9 linajengwa eneo la hali ya hewa ili kuongeza msukumo wa maji katika Kata hii ya Saranga na pindi mradi utakapokamilika basi adha ya maji itabaki kuwa historia" ameeleza Mhandisi Massaga.







Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages