Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Stanslaus Nyongo amewasili nchini Ubeligiji kuongoza ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Bajeti la Umoja wa Ulaya linalofanyika mjini Brussels nchini Ubeligiji kuanzia tarehe 20 hadi 21 Mei, 2025.
Tanzania imealikwa katika kongamano hili kama nchi pekee kutoka Afrika kushiriki katika kongamano hili kutokana na mahusiano mazuri ya muda mrefu na Umoja wa Ulaya.
Katika kongamano hilo ujumbe wa Tanzania utatatoa maoni kuhusu mwelekeo wa vipaumbele vya bajeti ya EU kwa kipindi kijacho hususan katika maeneo yanayogusa maendeleo endelevu, uwekezaji, na ushirikiano wa kimaendeleo na nchi za Afrika.
Mbali na kushiriki katika kongamano hilo, Mhe. Nyongo ataongoza pia ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa Afrika na Umoja wa Ulaya Mkutano huu muhimu unalenga kujadili masuala ikiwemo ulinzi na usalama, ustawi wa kiuchumi, , ushirikiano wa kimataifa na masuala ya uhamiaji.