Breaking

Thursday 24 February 2022

PAPA FRANCIS ATANGAZA MACHI 02, 2022 KUFUNGA NA KUIOMBEA UKRAINE




Kufuatia kile kinachoendelea baina ya Urusi na Ukraine, Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis amesema hatari ya vita ilmesababisha maumivu makali moyoni mwake.

Ametoa wito kwa watu wote kutumia siku ya Machi 2, 2022 ambayo ni Jumatano ya Majivu, kufunga na kuiombea Ukraine.

Ripoti zinaonesha tayari Russia imeanza kuishambulia Ukraine. Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine, Dmytro Kuleba amesema watashinda vita hivyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages