Breaking

Thursday, 24 February 2022

WAANDISHI WA HABARI WAWILI WAKAMATWA ARUSHA WAKIFUATILIA TUKIO LA ASKARI KUDAIWA KUPIGA RAIA



WAANDISHI wawili wa habari mkoani Arusha, Victor Korumba Moshi wa Global TV Online na Alphonce Kusaga wa Triple A Radio, wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani humo katika Kituo cha Polisi Azimio.

 

Waandishi hao wamekamatwa leo Alhamisi, Februari 24, 2022 wakati wakiwa wanatimiza majukumu yao ya uandishi wa habari.

 

Taarifa za kushikiliwa kwa wanahabari hao zimethibitishwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Wanahabari Arusha, Edwin Soko ambaye amesema wamekamatwa wakati wakifuatilia tukio la askari wa Kituo cha Polisi Sakina kudaiwa kuwapiga raia hapo jana, Februari 23, 2022.


Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi..!

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages