Breaking

Sunday, 27 February 2022

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI TPC



Na Samir Salum

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan amemteua Brigedia Jenerali Yohana Ocholla Mabongo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus leo Jumapili Februari 27,2022 kutokea Dubai amesema kuwa Brigedia Jenerali Yohana Ocholla Mabongo ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Uteuzi wa Brigedia Jenerali Yohana Ocholla Mabongo umeanza Februari 24,2022.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages