Breaking

Sunday, 27 February 2022

SERIKALI KUWAREJESHA WATANZANIA 300 KUTOKA UKRAINE


Na Samir Salum

Serikali imeanza kuchukua hatua za kuwarejesha nchini Watanzania takribani 300 waliopo nchini Ukraine kutokana na hali ya usalama kuendelea kuzorota nchini humo.


Katika taarifa iliyotolewa leo Jumapili Februari 27, 2022 na Mkurugenzi  wa  mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Emanuel Buhohela imesema kuwa hatua zinazoendelea kuchukuliwa ni pamoja na kuwaondoa hadi nchi jirani za Polandi na Romania ambako kuna utulivu.


“Hatua hii itatoa fursa kuwawezesha raia wetu kurejea nchini kwa usalama,” amesema Buhohela katika taarifa kwa vyombo vya habari.


Hatahivyo, serikali imesema hadi sasa hakuna Mtanzania aliyepata madhara kutokana na kile kinachoendelea Ukraine.


Aidha,  watanzania wenye ndugu jamaa pamoja wanafunzi wanaosoma nchini ukraine kuendelea kuwa watulivu katika kipindi hiki na kueleza kuwa itaendelea kutoa taarifa mara kwa mara.




Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages