Breaking

Saturday 26 February 2022

RAIS WA UKRAINE AVAA GWANDA NA KUINGIA VITANI, WANAJESHI 3500 WA URUSI WAUAWA



Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky leo amevaa Gwanda za Jeshi na kuingia "Uwanja wa Vita" kutetea nchi yake.

kulikuwa na tetesi kuwa Rais huyo amekimbia nchi, alijitokeza na kuomba Wananchi wapuuzie taarifa hizo akisema kufa na kupona watapambana na Urusi mpaka hatua mwisho.

Rais Volodymyr Zelensky amekataa ofa ya Marekani ya kumsaidia kuondoka Ukraine ili kuokoa maisha yake wakati majeshi ya Urusi yakiwa yameuzingira mji huo ambapo amenukuliwa akisema

"Mapambano yamefika. Nahitaji risasi, sio msaada wa kuondoka"

Mapema leo Asubuhi ya leo Jumamosi Februari 26, 2022 Maafisa wa Ukraine wamedai kuwa Urusi ilipoteza takriban wanajeshi 3,500 katika siku mbili za kwanza za vita kati ya mataifa hayo mawili.


Maafisa Wakuu wa Jeshi la Ukraine walitoa chapisho kwenye Facebook kwamba kulingana na makadirio yake, Urusi imepoteza ndege 14, helikopta nane, vifaru 102 na magari mepesi 536 ya kivita.

Mykhailo Podoliak, mshauri katika serikali ya Volodymyr Zelensky, alinukuliwa na vyombo vya habari vya Ukraine akisema wanajeshi 3,500 wa Urusi wameuawa katika mapigano hayo na karibu 200 wamechukuliwa mateka.

SOMA



Urusi bado haijakubali hasara moja ya mapigano katika operesheni ya Ukraine.

Wafanyikazi Mkuu wa Ukrain walisema Urusi "ilianza kuhamisha vitengo vya akiba katika mpaka na mikoa ya Ukraine na inaendelea na mashambulio ya anga katika viwanja vya ndege, ikipanga vikosi vya Wanajeshi wa Ukraine mashariki mwa Ukraine na kaskazini mwa mkoa wa Kyiv".

Maafisa wa polisi wamedai kuwa Urusi ilifanya mashambulio ya anga huko Odessa na kwa miundombinu ya kiraia huko Kyiv.

Endelea kufuatilia Lango la habari kwa taarifa zaidi.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages