hayo yameelezwa leo Jumatatu Februari 28, 2022 na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi katika mkutano wake na waandishi wa habari Ikulu ya Zanzibar na kueleza kuwa Serikali inafanya mpango kuhakikisha raia hao wanaendelea kuwa salama.
“Taarifa nilizokuwa nazo kuna watalii kama 900 kutoka Ukraine wapo Zanzibar na hawawezi kuondoka kurudi kwao licha ya muda wao kuendelea kuwa nchini kuisha lakini hawawezi kuondoka kwasababu ya hali ya kivita ambayo ipo nchini mwao,” amesema Dk Mwinyi
Amesema “Wameomba msaada ili Serikali iweze kuwasaidia kwasababu hawawezi kuendelea kukaa kwenye hoteli walipokuwa kwasababu hawana fedha. Lakini tumeanza mazungumzo na wenye hoteli kwa pamoja kuangalia jinsi ya kuwasaidia watu hawa wakati Serikali yao ikifanya mpango wa kuleta msaada.”
Dk Mwinyi amesema yapo makubaliano ambayo yameanza kuonekana na namna ya kuwasaidia hivyo mwisho watapata muafaka.
Amesema baada ya kupata muafaka na hatua watakayofikia Serikai itaeleza kitu gani kitafuata.
Amesema wanafanya hivyo kwasababu eneo hilo ni muhimu na mahususi kwa Serikali ya Zanzibar kibiashara.