Breaking

Wednesday, 16 March 2022

AMUUA MKE NA MTOTO WAKE NA KUWACHOMA MOTO KISA GUNIA ZA MPUNGA




 Jeshi la Polisi Mkoani Katavi  linamshikilia  Dutu Maige (30) kwa tuhuma za kumuua mke na mtoto wake mwenye umri wa miezi minne kwa kushirikiana na Yusuph Sitta (32).


Akithibitisha kutokea tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ally Makame Hamadi amesema kuwa walipokea taarifa Machi 8, 2022 kutoka kwa Paschal Masheku mkazi wa kijiji cha Sante Maria ambaye ni baba wa marehemu na kueleza kuwa binti yake alitoweka katika mazingira ya kutatanisha tangu Julai 2021 akiwa amebeba mtoto wake.


Kamanda Hamad amesema baada ya taarifa hiyo walianza upelelezi wa kina ambapo Machi 9, 2022 walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao waliohusikana na tukio hilo ambapo mmoja wao ni mume wa marehemu.


Ameeleza kuwa miili ya marehemu hao ilikutwa kwenye pori ikiwa imeharibika kwa kushambuliwa na fisi na baadae ilifanyiwa uchunguzi na madaktari wa magereza kwa kushirikiana na jeshi la polisi.


Amesema baada ya uchunguzi miili hiyo ilizikwa na jeshi la polisi ambapo baada ya mazishi watuhumiwa hao warirudi tena na kufukua miili ya marehemu kisha kuichoma moto na kuipeleka sehemu nyingine ili kupoteza ushahidi.


Kamanda ameeleza chanzo cha tukio hilo kuwa mme na mke walikuwa wakigombea mpunga ambao ni gunia 60 na walikuwa wakishtakiana mara kwa mara kwa watendaji wa kijiji ili kujua nani mmiliki halali wa mpunga huo.

Aisha Kamanda Hamadi amesema kuwa baada uchunguzi kukamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages