Breaking

Monday 7 March 2022

ATHARI ZA VIKWAZO DHIDI YA URUSI KWA UCHUMI WA DUNIA





Shirika la Fedha Duniani (IMF) limetangaza kuwa vikwazo dhidi ya Russia vitakuwa na athari mbaya na kubwa kwa uchumi wa dunia na kwa masoko ya fedha ya kimataifa na kwamba athari hizo zitaenea kwa kasi katika nchi nyingine.

Shirika la habari la Tass limeripoi kuwa, shirika la IMF limeeleza kuwa vikwazo viliyotangazwa dhidi ya Benki Kuu ya Shirikisho la Russia vinazizuia benki kutumia akiba yake ya fedha kwa ajili ya kuimarisha sarafu ya kitaifa na mfumo wa fedha wa nchi hiyo.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa, vikwazo vya kimataifa kwa mfumo wa kibenki wa Russia vinazuia pakubwa benki za nchi hiyo kutumia mfumo wa kimataifa wa mabadilishano ya kifedha SWIFT na kutatiza uwezo wa Russia wa kupokea fedha za mauzo yake ya nje na kulipia bidhaa kutoka nje sambamba na kufanya miamala ya kifedha nje ya nchi.

Aidha, Kutokana  vikwazo hivyo dhidi ya Urusi umeelezwa kuwa vitakuwa na athari kwa uchumi wa dunia kwa masoko ya fedha ya kimataifa.

Rais wa Russia, Vladimir Putin Alkhamisi tarehe 24 Februari aliamuru operesheni maalumu ya kijeshi katika eneo la Donbass kujibu ombi la msaada wa kijeshi kutoka kwa viongozi wa Jamhuri za Donetsk na Luhansk huko Mashariki mwa Ukraine. 

Russia imekuwa ikilalamika kwa muda mrefu kuwa, serikali yenye misimamo ya Kimagharibi ya Ukraine inalenga kujiunga na muungano wa kijeshi wa NATO unaoongozwa na Marekani na hilo ni tishio kubwa kwake.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages