Breaking

Tuesday 29 March 2022

DR CONGO YAJIUNGA RASMI JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI




Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wameipitisha rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mwanachama ndani ya umoja huo uliokuwa unaundwa na nchi sita.

DRC imepitishwa leo Jumanne Machi 29, 2022 katika mkutano wa 19 wa wakuu wa nchi wa EAC uliofanyika kwa njia ya mtandao chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta

Akitangaza rasmi Kenyatta amesema ni jambo la kihistoria kufanyika katika Ukanda wa Afrika Mashariki.

"Kukubaliwa kwa DRC kunaashiria tukio muhimu katika historia ya ushirikiano wa eneo hili!,” amesema Kenyatta.

Mwezi Disemba mwaka 2021, wakuu wa Jumuiya hiyo walipokea ripoti ya uhakiki wa utayari wa DRC kujiunga na EAC na kuwataka mawaziri wa Jumuiya hiyo kuharakisha mchakato wa majadiliano ya mkataba ili kuiwezesha DRC kuwa mwanachama na kuiwasilisha mapema mwaka wa 2022 wakati wa mkutano wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo.

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inakuwa nchi ya saba kujiunga na Jumuiya hii ikiwa ni nchi inyoongoza kwa idadi kubwa ya watu ndani ya nchi zilizopo EAC, ikiwa na watu takribani Milioni 92 jambo litakalopanua mzunguko wa biashara na upatikanaji wa masoko ya bidhaa zinazozalishwa ndani ya Jumuiya.

Lakini pia Tanzania itanufaika hasa katika ukuaji wa matumizi ya bandari, jambo litakalo chochea ukuaji wa uchumi nchini Tanzania pamoja na nchi zilizo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Kiusalama, DRC kudhiriwa kuwa ndani ya EAC itasaidia sana mapambano dhidi ya makundi ya waasi ambao wamekuwa wakitajwa kujificha ndani ya misiti mikubwa DRC na kuzishambulia nchi kama Rwanda na Uganda.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages