Breaking

Sunday 13 March 2022

KIWANDA CHA GSM CHAWAKA MOTO




Kiwanda cha kutengeneza magodoro kinachomilikiwa na Kampuni ya GSM kilichopo eneo la Mikocheni (karibu na Cocacola) Jijini Dar es Salaam kimeungua moto , bado chanzo cha moto huo hakijajulikana.



Kamishna Msaidizi wa Zimamoto Kinondoni (ACF) Christina Sunga amethibitisha kutokea kwa ajali ya moto na kuongeza kuwa moto huo ulioanza leo Jumapili Machi 13, 2022 saa 12:50 asubuhi bado unaendelea kudhibitiwa na sasa umezimwa kwa asilimia 80.

"Baada ya kupata taarifa hiyo tulifika haraka eneo la tukio, tukaomba msaada kwa wenzetu wa bandari na kampuni binafsi wanaohusika na shughuli za uzimaji moto", amesema.


Kamanda Sunga amesema hakuna taarifa yeyote ya majeruhi na mpaka sasa bado thamani halisi ya hasara iliyopatikana bado haijajulikana.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema moto huo umedhibitiwa na haujaleta madhara makubwa.

“Nampongeza kamanda mwenzangu wa zimamoto pamoja na vikosi vingine vilivyoshiriki, kazi imekwenda vizuri wamejitahidi hatujapata madhara mengine zaidi ya hili eneo” Kamanda Muliro

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: + 255 621 615 613 au +255 621 896 990

Pages